SIMBA KUONDOKA TANZANIA JUMANNE
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba, wanatarajia kuondoka Jumanne ijayo kwenda Algeria kupambana na JS Saoura katika mwendelezo wa michuano hiyo ambayo kwa sasa ipo hatua ya makundi.
Katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa Machi 9, mwaka huu nchini Algeria, Simba itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuitandika timu hiyo mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally ameliambia Championi Ijumaa kuwa: “Maandalizi kwa ajili ya safari yetu ya Algeria yanaendelea vizuri na kama mambo yatakaa sawa basi Jumanne ijayo tutaondoka kwenda huko.
“Hata hivyo, kwa sasa sijawa na uhakika kwa asilimia mia moja kwa sababu bado tunaendelea na utaratibu wa safari hiyo lakini kwa harakaharaka inaweza ikawa siku hiyo.”
Simba inahitaji ushindi katika mchezo huo ili ijitengenezea mazingira mazuri ya kutinga robo fainali.
Kwa sasa Simba inashika nafasi ya pili katika Kundi D ikiwa na pointi sita wakati Al Ahly ya Misri inaongoza ikiwa na pointi saba. JS Saoura wana pointi tano nafasi ya tatu, huku AS Vita ya DR Congo inaburuza mkia hilo ikiwa na pointi nne.
0 COMMENTS:
Post a Comment