March 3, 2019



KOCHA wa Stand United, Amars Niyoganbo ameiangalia Simba inavyogawa dozi kwa wapinzani, akageuka kuwatazama mashabiki akawaona wanakula kiporo, akatingisha kichwa akasema leo hamtoki Kambarage.

Stand United wataikaribisha Simba ambayo imetoka kuvunja mwiko wa kushindwa kufurukuta mbele ya Lipuli FC ya Matola mchezo utakaochezwa Uwanja wa CCM Kambarage.

Niyoganbo amesema anawatambua wapinzani wake vizuri kutokana na uzoefu wake ndani ya ligi pamoja na mbinu mpya alizowapa wachezaji wake lazima wabaki na pointi tatu.

"Kwa sasa tumejipanga kupata pointi tatu hizo ndio hesabu zetu, tumeanza kwa kasi na tutabaki kwenye kasi hiyo kwani timu yetu haipo kwenye mwenendo mzuri hasa kwenye msimamo tupo kwenye harakati za kuona tunaendelea kubaki ligi kuu.

"Wao wameshinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Lipuli nasi tuliipiga Lipuli, hatuna haja ya kuiogopa timu bali tunaiheshimu, walitufunga awali mabao 3-0 tulikuwa hatuna kikosi kipana ila kwa sasa Stand United ni habari nyingine," amesema Niyoganbo. 

Stand United wapo nafasi ya 13 wakiwa wamecheza michezo 28 na pointi 33 huku Simba wapo nafasi ya tatu wamecheza michezo 19 wana pointi 48 watacheza na Simba kwenye Uwanja waliotumia kuichinja Yanga kwa mara ya kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic