March 3, 2019


BEKI anayetisha kwa umbo ndani ya Simba, Pascal Wawa amesema kuwa kikubwa kinachowapa nguvu ya kuviparamia viporo kwa mafanikio ni utulivu walionao ndani ya kikosi cha Simba.

Simba imecheza mechi tano na imebeba pointi tatu kibabe huku ikitupia mabao 13 na kufungwa mabao mawili pekee kwenye michezo waliyocheza mpaka sasa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema wanatambua matokeo wanayoyapata kwa sasa ni mpango mkakati endelevu ulio ndani ya timu kwa sasa kutokana na ushindani kuwa mkubwa na kila timu kupigia hesabu pointi tatu.

"Sio kazi rahisi kufikia hatua hii, ushindani ni mkubwa hivyo kinachotusaidia kupata matokeo ni nidhamu kwa timu zote ambazo tunacheza nazo.

"Kila mchezaji anatambua wajibu wake na majukumu yake hali inayosaidia kuwa na mwendelezo chanya, namshukuru Mungu kwa sasa hatujafungwa mabao mengi hivyo tunapambana ili tuendeleze kufanya maajabu," amesema Wawa.

Simba imecheza michezo 19 ina pointi 48 na inashika nafasi ya tatu, ilianza kushinda mbele ya Mwadui kwa bao 3-0, ikaifunga Yanga bao 1-0, Lyon ikapigwa 3-0 kabla ya kuipa kipigo Azam FC 3-1 na kumalizia na Lipuli kwa mabao 3-1 leo ipo kazini kumenyana na Stand United Shinyanga Uwanja wa Kambarage.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic