March 4, 2019


WALE wabunge wanne walioteuliwa hivi karibuni na tawi la Wabunge wa Yanga Bungeni Dodoma kutoa ufumbuzi wa uchaguzi ndani ya klabu hiyo, wiki hii wamekuwatana kwa mara ya pili kuanza mikakati ya uchaguzi.

Yanga ambayo inahitaji kufanya uchaguzi mkuu wake wa kujaza viongozi baada ya wale waliokuwepo madarakani kujiuzulu akiongozwa na mwenyekiti, Yusuph Manji, ipo katika mchakato wa kufanya uchaguzi upya baada ya ule wa awali uliokuwa ufanyike Januari 13 kuahirishwa.

Miongoni mwa wabunge walioteuliwa hivi karibuni kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kamati ya uchaguzi ya TFF ni pamoja na Venance Mwamoto, Seifu Hamisi Gulamali, Dastan Kitandula na Saidi Mtanda ambao kwa sasa wapo katika mchakato wa kuandaa uchaguzi wa klabu hiyo baada ya ule wa awali kuvunjika.

Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Siza Lyimo amesema kuwa, tayari wabunge hao wameshakutana mara mbili katika vikao viwili ikiwa ni muendelezo wa vikao vyao ili kupata muafaka wa uchaguzi ndani ya klabu hiyo.

“Kamati ya wabunge wanne walioteuliwa kwa ajili ya kuandaa mchakato wa uchaguzi wamekutana siku ya Jumanne ikiwa ni kikao chao cha pili tangu kuundwa kwa kamati hiyo ambapo wakati wowote itatangaza tarehe ya uchaguzi kulingana na kile wanachokipanga hadi mambo yatakapokaa sawa,” alisema Lyimo.

Uchaguzi wa Yanga uliokuwa ufanyike Januari 13 ulivunjika kufuatia baadhi ya wanachama kupinga uchaguzi huo mahakamani jambo ambalo lilisababisha uahirishwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic