March 4, 2019


Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilali 'Bilo' amemtupia lawama Mwamuzi wa mechi ya jana dhidi ya Simba waliyochapwa kwa mabao 2-0.

Akizungumza mara baada ya mchezo, Bilo alieleza kuwa Mwamuzi aliwabeba na kuwasaidia Simba kupata mabao 2 ambayo alidai hayakuwa halali.

Kocha huyo ambaye alitamba kuwamaliza Simba kwenye kipute hicho, anaamini Mwamuzi aliwapa msaada Simba na mechi haikuwa na usawa kiuchezeshaji.

"Tumefungwa lakini Mwamuzi amewasaidia Simba, si mabao sahihi kwakuwa kulikuwa na upendeleo kwao",

"Naweza kusema msaada wa refa umewasaidia Simba kuchukua alama tatu ambazo si halali kutokana na namna mchezo ulivyochezeshwa" alisema.

5 COMMENTS:

  1. Huyu nae aache utundu Lisu yaai hovyo kabisa.kwani kama kweli refa angechezesha kwa haki basi kipa wa stand United alistahiki kupewa kadi nyekundu na Simba kuzawadiwa penalty kwa faulu aliokwenda kumchezea Rashid Juma wa Simba.Na vile vile refa aliashiria faulu kwa kagere wakati akielekea langoni kwa stand United kwenye mpira ambao ulikuwa 50/50 kati yake na mchezaji wa stand na kagere akafanikiwa kuumiliki mpira faulu ile rafa kaitowa wapi? Katika mchezo na stand Simba wamenyimwa kama penalty tatu za wazi. Ball position Simba akimiliki kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka mpira unamalizika nafasi ya stand ya kuishinda simba ilikuwa wapi? Kama makocha wetu wenyewe ndio hawa basi kipindi si kirefu timu zetu zitaajiri makocha kutoka sudani ya kusini yaani hovyo kabisa hata Zahera timu yake ya Yanga iliyoipa changamotoya Simba alikiri timu yake kuzidiwa kiwango na Simba pale kwa mkapa, sisi watanzania laana ya kohofia kuzungumza ukweli alitulani ni nani?

    ReplyDelete
  2. Tena angejua walikuwa wapigwe zaidi ya tatu kama siyo mwamuzi kuwasaidia Stend united!!vipi penalty iliyonyimwa Simba?

    ReplyDelete
  3. SIMBA WALIKUWA NA NAFASI YA KUWAPIGA GOLI 4 STAND MUMSHUKURU SANA REFA AMEJITAHIDI SANA KUCHEZESHA. KAMA ANGEWABEBA SIMBA MCHEZAJI WENU ALIPO SHIKA MPIRA KIPINDI CHA KWANZA INGEKUWA GOLI, RASHID JUMA ALIPOANGUSHWA NDANI YA ENEO LA PENETI AKACHUPA REFA KAIONA LAKINI ANGEWEZA KUAMUA IWE PENETI, DAKIKA 10 ZA MWISHO SIMBA HAWAKUTAKA KUJIUMIZA WAKAWA WANAPOTEZA MUDA KWA KUWA NA MIPIRA NA KUPASIANA NA KUITOA KOCHA UNAJITETEA KITOTO SANA MPIRA WOTE TUMEUONA BADO UNATAKA UTUAMINISHE REFA KAWAONEA SIO KWELI HATA CHEMBE

    ReplyDelete
  4. Ndio walimu wetu hawa wa mpira kabla ya kufungwa hoja huwa nyingine baada ya kufungwa huja na hoja yao kuu kuwa timu iliyo shinda wamenunua mechi niliona game ya lipuli jamaa alipo mpiga kiwiko John boko lakini kocha wa alisema refa kawaonea mchezaji wao

    ReplyDelete
  5. KOCHA HUYU ANAKULA MATAPISHI YAKE MWENYEWEW .... KASAHAU ALICHOKISEMA? ....Kocha wa klabu ya Stand United, Athuman Bilal 'Bilo', amesema mechi yao ijayo dhidi ya Simba ni ya kawaida mno.

    Simba na Stand zitakutana tena katika mchezo ambao utakuwa ni wa raundi ya pili ambapo Stand wakiwa na kumbukumbu ya kichapo cha mabao 3-0 kwenye Uwanja wa taifa.

    Bilo ametamba kuwa mechi dhidi ya Simba ni ya kawaida sana kama wanacheza na Lipuli, Ndanda, Singida United na timu zingine.

    Ameeleza kuiona Simba kama timu zingine akisema ina kikosi cha kawaida hivyo hawana presha kabisa kuelekea mechi hiyo.

    "Simba ni wa kawaida mno, sioni utofauti na timu zingine, tutawashangaza kama ilivyokuwa kwa Yanga wakija Shinyanga" alisema.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic