March 12, 2019

KOCHA wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike wiki hii alitangaza kikosi cha wachezaji 25 ambao wataikabili Uganda. Tanzania inajiandaa kucheza mchezo wa mwisho wa kufuzu Mataifa ya Afrika dhidi ya Uganda Machi 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam mechi ambayo ni muhimu na ya kihistoria.

Huo utakuwa ndiyo mchezo wa mwisho kwa Stars kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika ambayo yatafanyika Misri. Hivyo Tanzania inatakiwa kupambana kwa bidii nakuweza kuona inaibuka na ushindi kwani tayari Uganda imefuzu Kuna jambo moja ambalo lilijitokeza baada ya kocha Amunike kutaja kikosi chake.

Mashabiki na wadau wengi walionekana kutofurahishwa na baadhi ya wachezaji wao kutokuwa kwenye kikosi hicho. 

Maoni yake kulingana na uelewa wake wa kiufundi lakini yote kwa yote tunapaswa kuelewa kwamba Kocha ndiye muamuzi wa mwisho na ndiye aliyepewa dhamana ya kuiongoza timu hiyo.

 Huu siyo muda wa kulumbana ni muda wa kuungana na kusapoti wachezaji wetu kuhakikisha kwamba timu yetu inafuzu kucheza michuano hiyo. 

Tukianza migawanyiko na kunyoosheana vidole kwa misingi ya ushabiki wa timu hii na ile au mchezaji huyu na yule hatuwezi kujenga wala kufanya kitu cha maana.

Ni vyema mawazo ya kocha yakaheshimiwa sababu yeye ndiye anafahamu kwanini kamuita mchezaji fulani na mwingine kamuacha na yeye ndiye mwalimu ambaye amekabidhiwa rungu hilo na ni nia yake kufuzu vilevile
ili kujenga heshima yake na kujitangaza kimataifa.

Kocha amekabidhiwa majukumu hayo na taifa hivyo aungwe mkono na asinyooshewe vidole katika kazi yake zaidi apewe sapoti kwa nguvu zote. Watanzania tunajua mna mapenzi na soka na mnatamani kuona timu yenu inashiriki Afcon lakini si kwa kupiga kelele na kumkosoa mwalimu zaidi inahitajika sapoti kwa mwalimu kuweza kufi ka mbali.

 Tunaamini kikosi ambacho ametaja kocha Amunike kitakuwa msaada kwa taifa na kitafanya vizuri kwenye mchezo na Uganda.

Kila mmoja anapaswa kuelewa kwamba tunahitaji ushindi kwa namna yoyote ile ili kufuzu na kwa aina ya timu Uganda waliyonayo tunahitaji mshikamano mkubwa sana ndani na nje ya uwanja.

 Uganda ina wachezaji wenye uzoefu na ambao wanaijua vilivyo Tanzania hivyo tusipokuwa na mshikamano na kuondoa tofauti zetu tunaweza kukwama na kujikuta tukifedheheka na kuendelea kushangilia timu za wengine kila mwaka.

Huu ni wakati wetu na tuna kila sababu ya kufuzu kwavile kundi letu liko wazi na mechi yenyewe ya kufuzu inachezewa uwanjani kwetu mbele ya mashabiki wetu, hatuna sababu yoyote ya kutofanya vizuri. 

Kila kitu kipo mikononi mwetu. Hivyo ni vizuri Watanzania wakaheshimu kile ambacho kinafanywa na kocha Amunike sababu nchi ni yetu taifa ni letu tuungane kwa pamoja kuisapoti Star.

3 COMMENTS:

  1. MOHAMMED ZIMBWE JR TSHABALALA, AJIBU, DILUNGA KWAKWELI WALISTAHILI KUPEWA NAFASI TIMU YA TAIFA. CHUKI ZENU ZINAIGHARIMU TIMU YETU YA TAIFA.

    ReplyDelete
  2. Amunike hapigiki tafu yaani sio rahisi watanzania kuwa na imani nae hivi sasa. Labda Amunike na wapambe wake wanawachukulia watanzania kirahisi rahisi tu katika ufahamu wao kwenye mpira. Kosa alilolifanya Amunike kule Lesotho ndilo analoendanalo kwenye mechi ya Uganda.Atanzaje figisu na wachezaji wazoefu na kuwaacha kwa kisingizio cha nidhamu alafu anasema hata timu ikifungwa kwake yeye sawa kwani kikubwa anachoangalia ni nidhamu anasahu yakwamba nidhamu ya kwanza kwa mchezaji ni uwezo wake uwanjani na sio kumuogopa kocha. Nadhani hata waafrica kusini wanacheka kwa dharau kwa timu ya taifa ya Tanzania kumuacha machezaji kama Banda kwani kwa wachezaji gani hasa Tanzania tulionao wenye viwango kaliba ya Banda hata asiitwe timu ya taifa? Na tutake tusitake kwa sasa ukiachana na wachezaji wanaocheza nje ya nchi ni timu moja tu nchini yenye wachezaji waliokumbana na mazingira magumu na changamoto ya high level ya soka la Africa nayo ni Simba peke yake. Kama ningekuwa Amunike ningehakikisha kwa kila mchezaji wa Simba anaepata namba kwenye mashindano ya club bingwa Africa namjumuisha kwenye timu ya Taifa. Khasani Dilunga,Rashid Juma,Shabalala,Mzamiru. Sio tu kwa upenzi bali hawa ni wachezaji ambao wapo kwenye mazingira ya mashindano makubwa ya kimataifa hivi sasa na wanafanya vizuri. Ukiangalia nafasi ya uzoefu wanaoipata wachezaji wa Simba hata hao wengi wa wachezaji walioitwa wanaocheza nje ya nchi hawaipati. Simba inapambana na club kumi na tano 15 bora barani Africa na katika kundi lake lina club namba moja barani Africa sisi watanzania alieturoga ni nani mpaka tunashindwa kung'amua ukweli wa vitu vidogo tunakwenda kupumbazwa na jina la mtu kufanya vitu anavyotaka yeye hata kama anakosea. Ukiachana na Ulimwengu kuna mchezaji mwengine wa kitanzania anaepata namba kwenye kuwakilisha timu yake club bingwa Africa? Raisi Magufuli alishafunga mjadala kwa kusema msidhani watanzania ni wajinga saaana.

    ReplyDelete
  3. كثيراً ما يضيّع الإنسان الكثير من وقته في قراءة كتاب غير مفيد، أو قراءة كتاب صعب بينما هناك الأسهل، أو كتاب سطحي بينما هناك الأعمق.
    مدافن للبيع
    مقابر للبيع
    تحميل واتساب الذهبي
    مقابر للبيع
    خبير سيو
    مصمم ديكور

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic