April 26, 2019


Baada ya Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwashutumu vikali wachezaji wake jana baada ya kushindwa kufanya mazoezi kisha mishahara, Beki wa timu hiyo, Haji Mwinyi amesema hawakugoma.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha Spoti Leo, Mwinyi amefunguka akisema kuwa kwa sasa wanapambana kwa ajili ya kuchukua kikombe cha ligi na hawana haja ya kugomea.

Ameeleza kuwa hawawezi kamwe kumwangusha Zahera kwani wanamuheshimu na wanathamini kazi yake ndani ya timu hivyo yanayosemwa kuwa hawakufanya mazoezi hayakuwa na uhakika.

"Hakuna ukweli bwana, sisi tulifanya mazoezi kama kawaida.

"Yanayosemwa wala hayana ukweli maana kwa sasa tunapambana kwa ajili ya kusaka ubingwa.

"Hatuwezi kumwangusha Kocha wetu kwakweli, tunamheshimu mno na hilo haliwezi kujitokeza kabisa, hatujagoma," amesema Mwinyi.

Wakati Zahera akilalamikia suala hilo, Yanga hivi sasa inapaswa kuendelea kujifua vilivyo kwani itakuwa inakabiliana na Azam FC katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Jumatatu ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

5 COMMENTS:

  1. Mimi sijaelewa vizuri hapa, labda aliyeelewa anisaidie. Ina maana zahera yupo kwingine na timu ipo kwingine? Maana kocha anasema wachezaji wamegoma mchezaji anasema hawajagoma au stori imetungwa? Naomba kujuzwa maana sie watu wa pembezoni hatuna source nyingine zaidi ya hii.

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa anachanganyikiwa vibaya huku akimfukuza kila anaedai haki zake na huku akimvaa Manara ambaye hamuwezi kwa hoja na huku akisema hawataki wachezaji wa Simba na huku akiwaania kutaka kuwasajili na inazidi hali yake ya kujikanganya kila anapomuona mnyama yupo nyuma yake akijiona yuko mbali na ubingwa

    ReplyDelete
  3. Wanatuchanganya Sasa kila mtu anasema lake Sasa ukweli ni upi ,ila nilivyo fuatilia taarifa nyingi zinaonesha wamegomemea mazoezi,Sasa naona mchezaji anatutia moyo ,mim naona wawe wazi maana club yetu ipo katika wakati mgumu kifedha kuliko kutudanganya ,huyu anasema hivi na huyu anasema hivi.Tuwekeni sawa.

    ReplyDelete
  4. Muda mwingi Yanga wameutumia kuwa kwenye vyombo vya habari.....wakati Azam, Simba na timu nyingine muda wao mwingi wameuweka kwenye matayarisho na maandalizi ya mechi (kimwili na kisaikolojia).....sijui ni kwanini????Kocha Mwinyi Zahera wekeza muda wako kufundisha mpira....hiyo jumatatu sijui itakuwaje hapo jangwani baada ya mechi Azam vs Yanga?

    ReplyDelete
  5. Ni kufukuzana ndio itakuwA Jangwani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic