April 26, 2019


MENEJA wa Meddie Kagere, Patrick Gakumba amewaambia viongozi wa Yanga iwapo wanahitaji saini ya mshambuliaji wa Gor Mahia wa Kenya, Jacques Tuyisenge wanatakiwa watoe kitita cha dola 200,000 ambazo ni sawa na milioni 460 za Kitanzania.

Yanga imeonyesha nia ya kumsainisha Tuyisenge baada ya kumpigia simu meneja huyo kwa kumtaka ataje dau la mchezaji huyo ili wafanye mchakato wa kumsajili. Hata hivyo ukiachana na Yanga pia Simba ndio walioonekana kuanza kuzungumza na meneja huyo kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye kiwango cha juu ambapo inavyoonekana mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama.

Gakumba alisema kuwa, mara baada ya viongozi wa Yanga kumpigia simu aliwatajia dau la Tuyisenge ambalo ni dola 200,000 ambapo bado hawajafikia muafaka. “Viongozi wa Yanga walinipigia walitaka niwatajie dau ninalolihitaji kwa ajili ya Tuyisenge na nikawatajia kuwa ni dola 200,000 lakini bado hawajanirudishia majibu nasubiria majibu kutoka kwao.

“Iwapo watafanikiwa kutoa kiasi hicho cha fedha basi nitakuwa tayari kumuachia ikiwa ni pamoja na kumuhakikishia mazingira mazuri ya kazi,” alisema Gakumba. Lakini habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinadai kwamba aliwatajia bei ya kuwakomoa ila wakikaa mezani rasmi huenda ikapoa kwa kiasi kikubwa.

4 COMMENTS:

  1. Kila la kheri Yanga. Million mia mbili unakwenda Burundi ubapata vifaa vinne vya maana kwa million 40 zako na change inabaki.

    ReplyDelete
  2. Zidi kutembeza bakuli heenda zikapatikana na kuhusu mishahara yake na mishahara ya wengine wanaotakiwa usiuogope mwachieni Mungu

    ReplyDelete
  3. Hapo sasa dola 200,000 sawa na milioni 400 na zaidi halafu tunapeana imani atakuja Yanga hizi kauli za kampeni tu, tunapimwa saizi ya viatu leo halafu kesho unaulizwa ulikuwa unataka viatu gani na gani loo hii ndio TZ bwana!

    ReplyDelete
  4. Huh utakuwa uwendawazimu kwa klabu yeyote hapa nchini wetu Tanzania kumnunua huyu mchezaji wa Gormahia kwa dau kubwa hivyo. Hana umuhimu na umaarufu mkubwa hivyo. Tumieni pesa venu vizuri achaneni na hawa wapiga madili makubwamakubwa bila viwango vya uchezaji kulingana na pesa ndefu. Simba na Yanga hamna ulazima wa kufuja pesa venu kwa huyo anayetaka kuzikamua klabu zetu za Tanzania.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic