KOCHA wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa kwa hasira walizonazo kwa sasa lazima waanze kumchapa Simba ili waongeze kasi ya kubaki ligi kuu na kuheshimiwa na wapinzani.
Biashara United haipo kwenye nafasi nzuri kwa sasa kwani imecheza michezo 31 ikiwa nafasi ya 19 ina pointi 34 kibindoni zinazoiweka kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja msimu ujao.
Sai amesema"Hatupo kwenye nafasi nzuri kwa sasa, naona Simba wanavyokuja kwa kasi na spidi yao naiona ila hiyo hainipi mashaka kwa kuwa naitambua vizuri Simba ni lazima nishinde mchezo wangu wa leo.
"Nikishinda mchezo wangu mbele ya Simba itaongeza morali kwa vijana kuendelea kupambana kwenye michezo yetu inayofuata hali itakayotufanya tubaki ligi kuu msimu ujao na tayari tumeanza kuiwinda Simba na michezo inayofuata," amesema Said.
Simba itamenyana leo na Biashara United uwanja wa Karume majira ya saa 10:00 jioni.








kamuulize kmc kaka labda uwaambie wachezaji wako mpira hata tumboni usiwaguse otherwise jioni utakuja na kauli nyingine
ReplyDelete