April 27, 2019


MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Obrey Chirwa, ameweka wazi mikakati yake kuhusiana na mechi ya Jumatatu ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.

Azam FC itapambana na Yanga katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambao utakuwa ni wa kwanza wa ligi hiyo kuzikutanisha timu hizo msimu huu.

Chirwa amesema kuwa, mikakati yake aliyojiwekea kuhusiana na mechi hiyo ni kuhakikisha anaifunga Yanga.

Alisema atafurahi zaidi kama atafanikiwa kuifunga Yanga ambayo ilikuwa timu yake ya zamani katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Alisema furaha aliyoipata katika michuano ya Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar ambapo aliifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Azam iliupata ilikuwa ni ya kawaida kwa sababu alikifunga kikosi cha pili kilichokuwa na mchanganyiko wa wakongwe kidogo.

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu dhidi ya Yanga ambayo ni timu yangu ya zamani niliyokuwa nikiipenda.

“Lakini ikitokea hiyo Jumatatu nikaifunga Yanga nitafurahi sana kwani nitakuwa nimetimiza moja kati ya ndoto zangu ambazo nimekuwa nikiziota kila siku,” alisema Chirwa.

1 COMMENTS:

  1. Ukweli ni kwamba hakuna mazoezi na matayarisho ya nguvu waliyoyafanya Yanga wachezaji walipewa mapumziko ya sikukuu kwa siku 3 na siku ya 4 mpaka ya 5 walikuwa kwenye mgomo wameanza mazoezi jumamosi....hii ni hatari sana....kila mtu yuko bize na uchaguzi na kampeni ya michango!...wachezaji wanatokea nyumbani wakati Azam wameanza maandalizi tokea jumatatu....kila kitu kiko wazi....timu iliyofanya maandalizi inaonekana na isiyofanya maandalizi inaonekana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic