April 26, 2019


Kuna uwekezakano mkubwa wa kikosi B cha Yanga kikichanganyika na kile cha kwanza kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC Jumatatu ya wiki kesho.

Hii ni kutokana na mwendelezo wa wachezaji wa timu hiyo kuzidi kugomea mazoezi wakishinikiza walipwe fedha zao za mshahara ambazo wanadai.

Katika mazoezi ya jana wachezaji wa Yanga waligoma kutokana na madai hayo ya fedha zao pamoja na leo asubuhi huku wachezaji wa kikosi B wakihusika nayo pekee.

Wachezaji wa kikosi cha kwanza waliwasili kama kawaida kunako Uwanja wa Chuo cha Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam na kuishia kwenye magari yao huku wakishindwa kujifua kuelekea mechi hiyo.

Licha ya mgomo huo kutokea, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omar Kaya amesema kulikuwa na tofauti ya mawasiliano baina ya klabu na wachezaji lakini sasa wameshalimaliza.

Kaya ameeleza kuwa tatizo hilo limeisha na sasa wachezaji wao wataendelea na mazoezi yao kama kawaida tayari kwa mechi ya Jumatatu.

Kwa upande mwingine naye Nahodha Msaidizi wa timu hiyo, Juma Abdul naye amefunguka kuwa hakuna tatizo lolote lililopo baina ya wachezaji na timu hususani jana akisema kilichosababisha kutofanya mazoezi jana ilikuwa ni suala la muda.

"Nipende kuwatoa hofu washabiki na wapenzi wa Yanga kuwa hakuna mchezaji yeyote wa Yanga aliyegoma lakini ni kwamba tulitofautiana tu katika suala la muda.

"Sisi jana tulihitaji kuonanana na Uongozi wetu baada ya mazoezi kwa ajili ya ufafanuzi wa mambo machache lakini sisi tuliwahi kuondoka na wao wakaja baadae"


"Namshukuru Mungu leo tumekutana nao na tumezungumza".

3 COMMENTS:

  1. HIVI HAWA WACHEZAJI WANASAHAU? WAWAULIZE AKINA SUNDAY MANARA NA TENGA. TULISHATEMBEZA BAKORA PALE JANGWANI WACHEZAJI WAJUE THAMANI YA KLABU SIO KULETA MIGOMO YA UJANJAUJANJA. TUNAWAPENDA WACHEZAJI WETU MPAKA TUNAWACHANGIA ILA MSTUZINGUE.

    ReplyDelete
  2. Viongozi acheni ujanjaujanja timizeni mahitaji ya wachezaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic