April 25, 2019


WACHEZAJI wa zamani wa Simba kipa, Juma Kaseja na mshambuliaji, Elias Maguli leo wataiongoza KMC kuwavaa Wekundu hao Jijini Mwanza.

Simba itaingia uwanjani katika mchezo huo wakitoka kupata ushindi wa mabao 2-0 walioupata walipocheza juzi Jumanne na Alliance kwenye uwanja huo.

Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amesema siyo mchezo mwepesi kwao kutokana na ubora wa wapinzani wao katika mechi za hivi karibuni, hivyo ataingia uwanjani kwa tahadhari kubwa ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Aussems amesema kikosi chake kitakuwa na mabadiliko ya baadhi ya wachezaji ambao atawapumzisha kutokana na uchovu.

“Nimejaribu kutengeneza mzunguko wa wachezaji kucheza kwa zamu ili wapate muda wa kupumzika kutokana na mfululizo wa mechi tunazoendelea kuzicheza za ligi.

“Hivyo, ni lazima kikosi changu cha leo kitakuwa na mabadiliko kidogo ya wachezaji ambao hawakucheza mchezo uliopita na Alliance.

“Kuhusu maandalizi ya timu tupo vizuri, kikosi changu kinakabiliwa na majeruhi walewale Kapombe na Nyoni ambao wote wameanza mazoezi mepesi,”amesema Aussems ambaye wachambuzi kitakwimu wanampa nafasi kubwa ya kubeba Kombe.


Kocha Mkuu wa KMC, Etiene Ndayiragije alisema ; “Simba ni moja ya timu kubwa hapa nchini iliyokuwa na wachezaji wengi wenye uzoefu na uwezo mkubwa, lakini hiyo haitatufanya tuwahofie tutaingia uwanjani kwa ajili ya kupata ushindi.”

Kocha KMC, Ettiene Ndiyaragije amesema kuwa hana hofu na mchezo wa leo kwani amewaanda wachezaji wake kisaikolojia ana uhakika wa kubeba pointi tatu mbele ya Simba.

"Vijana wanajituma na wanapambana kupata matokeo, kila siku tunafanyia kazi makosa ambayo tumeyafanya ili kuwa bora zaidi, ni wakati wetu kuonyesha tofauti," amesema.

Mchezo wa mwisho KMC alitoka suluhu na Singida United uwanja wa Namfua Singida.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic