April 30, 2019


RAIS  John Magufuli ameeleza masikitiko yake kufuatia timu za soka za taifa ambazo ni timu ya wakubwa (Taifa Stars) na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys,  kufungwa na timu za mataifa mengine katika michuano mbalimbali ambayo imechezwa hivi karibuni.

Magufuli amesema hayo leo Aprili 30, 2019 wakati wakiwahutubia wananchi wa Kyela mkoani Mbeya ikiwa ni siku chache baada ya Serengeti Boys kuondolewa kwenye michuano ya Afcon U17, iliyokuwa ikichezwa hapa nchini na kusema  kitendo cha kufungwa kwa timu hizo kimekuwa kikimnyima raha huku akimtaka waziri wa micghezo, Dkt Harrison Mwakyembe kufuta aibu hiyo ya kufungwa kila mara.

“Kukatika kwa umeme kunaumiza sana, unakuta unaangalia mpira umeme unakatika halafu goli linaingia, na Waziri wa Michezo anatoka huku Mbeya, ingawaje kwenye timu ya vijana ameniangusha sana. Katika vitu ambavyo huwa vinaniudhi ni kufungwa timu zangu, huwa inaniuma mno, yani watu milioni 55, mnafungwa na timu ya nchi yenye watu milioni 33, hii ni aibu kubwa mno.

“Natamani siku moja niwe waziri wa michezo halafu niwaonyeshe mimi ni nani, kwanza kikosi nitakipanga mimi mwenyewe halafu tuone kama tutafungwafungwa tena, timu ya wakubwa nayo hivi karibuni itaanza mashindano, sijui nayo mechi ya kwanza tu itafungwa! Labda kufungwa nao ndiyo mchezo mzuri,” amesema Magufuli.

Katika michuano Afcon U17, Serengeti Boys wakiwa wenyeji wa michuano hiyo walitoka bila pointi baada ya kufungwa mechi zao zote tatu na kuaga mashindano hayo katika hatua ya makundi.


1 COMMENTS:

  1. Waache watu waseme wasemavyo ila Magufuli si mnafiki na ni jasiri kweli kweli kikauli na vitendo na kazi aliyojipa ya kuwa mpasua majipu kwa kweli anaitendea haki ingawaje Muheshimiwa raisi hapana shaka katika upasuaji wake huo wa majipu ikawa uchungu kwa watumbuliwa lakini kiufasaha kabisa hakuna mgonjwa wa jipu atakaepata nafuu bila ya kutumbuliwa jipu hilo. Ni wakati wa kueleza ukweli kabisa yakwamba kwenye timu yetu ya vijana U17 tumechemsha na vyema tukaa chini na kujadili kwa kina sababu ya kufeli huko badala ya wahusika kujaribu kufifirisha ukweli wa mambo. Mara nyingi tumekuwa tukitoa maoni yakwamba timu za vijana ndiko kwa kuekeza huko. Kwa kutafuta makocha wa viwango wenye uzoefu na makuzi ya vijana katika mpira kimataifa. Kuna wakati wadau wa mpira walipendekeza sana kuajiriwa kwa kocha aliewahi kuifundisha Simba na baadae kwenda kuifundisha Stand United ya shinyanga yule mzee wa kifaransa kuwa ndio kocha wa timu za taifa za vijana. Kama Stand United iliweza kumudu kuwa nae japo kwenye hali duni vipi taifa lishindwe? Yule Mzee wa kifaransa ni mtaalamu wa soka la watoto hata huyo Milambo angejifunza mengi kutoka kwake . Kuja kwa yule mzee hapa nchini ilikuwa ni nafasi ya pekee kupata kocha wa kutunyooshea makuzi ya vijana wetu katika soka na kuwa professional players wanaojitambua. Wapo waliosema kuwa kocha alikuwa mkali na asiekubali ushauri. Lakini kiuhalisia ukisikia mtanzania analalamika kuwa bosi wake ni mkali kazini basi ujue pana kiongozi hapo anaesimamia kazi yake vizuri. Viongozi wanaosimia mpira utaona kana kwamba wanalichukulia suala la mpira wa miguu kimzaha mzaha tu ila mpira wa miguu ni shughuli pevu inayohitaji ujasiri vile vile wa kujitoa kwa ajili ya taifa. Kama viongozi husika watachukulia mchezo wa mpira ni mchezo tu kama jina lake linavyosema kuwa ni mchezo basi tutachelewa sana kufika . Mpira ni biashara nzinto yenye kuhitaji uwajibikaji wa hali ya juu. Yenye kuhitaji ubunifu wa hali ya juu kwa viongozi wake . Lakini kikubwa zaidi ni uadilifu wa kazi kwa wahusika wanaoisimamia Taasisi inayosimamia mpira. Mpira ni biashara yenye ushindani wa hali ya juu duniani kwa sababu mara nyingi ni mchezo unaobeba taswira ya nchi fulani. Na ni ajira yenye kuunganisha mambo mengine mengi kama utalii,afya,habari nakadhalika.lakini yaonekana kama Nchi, bado hatuja amka na kuchangamkia sekta ya michezo ipasavyo kama platform ya kuitangaza nchi yetu Duniani. Au labda wahusika wenye dhamana wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.Na huwezi kujitangaza bila ya kufanya mambo makubwa ya mutengeneza habari za kuvutia. Kwa mfano kwenye U17 inayojulikana na kutangazika duniani ni Cameroon licha ya mashindano hayo kufanyika Tanzania. Na kwa mpira wa miguu asikwambie mtu cha kwanza cha kuzingatia ni kuwa na walimu wenye uzoefu na utaalamu wa kutosha kwa ngazi husika. Kwa mfano kocha wowote wa timu ya Taifa lazima awe ameshawahi kucheza mpira kwenye ngazi za kimataifa na ikiwezekana awe ameshapata mafanikio kadhaa katika kazi yake ya ufundishaji kwa ngazi ya kimataifa au klabu. Lakini kama tutaendelea kuteua makocha wetu wa timu za taifa kwa utashi wa watu fulani na si kwa vigezo stahiki vya kazi basi watanzania tutarajie kuendelea kupata maumivu. Na kwanini tusiwe na system ya kupiga plan ya kujenga gorofa hata kama mipango yetu ilikuwa ni kujenga kibanda? Viongozi wetu wanaosimamia mpira lazima wawe na mawazo mapana. Lazima wawe majasiri wa kujaribu kwani always,no risk no reward. Kwa maoni yangu wakati TFF inajiandaa kuandaa Afcon ya U17 basi huyu Amunike ndie alipaswa kuajiriwa kuwa kocha wa kuwaandaa hawa vijana wa Afcon kwani Amunike ni Kocha wa vijana . Kwa Amunike kupewa Taifa stars ni kumbebesha mzigo usio saizi yake kwani hata yeye mwenyewe amekiri kusema anahisi ni kama kapewa upendeleo fulani hivi kwa kupewa majukumu ya taifa stars. Anaweza kuwa anania njema kabisa ya kuisadia Tanzania bali kila kitu kina kiasi chake na kiasi kikizidi uwezo wa mtu basi there's nothing that can be done.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic