April 13, 2015


Pamoja na kwamba itakuwa inacheza ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Simba imesema haitaki masihara inataka ushindi tu.


Simba inataka kushinda mechi zake zote tano zilizobakia ikiwemo hiyo ya Aprili 18 dhidi ya Mbeya City.

Simba kwa sasa imeshacheza michezo  21 na ina pointi 35 na tayari awali ilishavaana na Mbeya City katika Uwanja wa Taifa na kupoteza mchezo kwa mabao 2-1.
 Mkurugenzi wa Kitendo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Haji Manara, alisema kuwa lengo lao ni kuondoka na ushindi Sokoine.

Manara alisema ili kuhakikisha wanafanya vyema, kikosi chao kitaanza kujiwinda mapema leo Jumatatu kabla ya kutimkia mkoani Mbeya.

“Simba imebakiza mechi moja mkoani ambayo  itacheza dhidi ya Mbeya City na sisi tunahitaji alama tatu katika mchezo huo na Kopunovic ameahidi kufanya maandalizi ya nguvu kwa vijana ilikuweza kuonyesha kuwa mchezo wa kwanza tuliteleza  tu.

“Kwa ujumla sisi kama klabu na mipango ya mwalimu ni  kufanya vyema  na kuibuka na ushindi, bila kujali awali tulipoteza,  safari hii tunakuja kivingine kabisa kuweza kupambana,” alisema  Manara.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic