April 25, 2019


UONGOZI wa KMC umesema kuwa upo 'siriazi' leo wanazipigia hesabu pointi tatu ili kujega heshima ya kikosi hicho chenye maskani yake Kinondoni.
KMC ambayo ilipanda daraja msimu huu wa 2017/18 mchezo wake wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 leo itamenyana na Simba CCM Kirumba.
Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa mchezo wao wa kwanza tayari umeshapita hata wakiukumbuka matokeo hayatabadilika kilichopo mbele yao ni mchezo wa leo.
"Unajua Simba ni timu kubwa na imepiga hatua kubwa kwa kushiriki ligi ya mabingwa sasa tukiwapiga tunajiwekea heshima na kuonyesha ushindani wa kweli kwenye ligi.
"Tumejipanga na tayari tupo sawa kwa ajili ya mchezo wetu, morali ni kubwa na kila mchezaji yupo tayari tunawaomba mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema Binde.
KMC ipo nafasi ya 7 ina pointi 42 ikiwa imecheza michezo 31 imepoteza michezo saba na kutoa sare michezo 15 na imeshinda 9.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic