April 25, 2019


KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameamua kuwachana wachezaji wake kwamba wanamuangusha kwa kushindwa kutimiza majukumu yao uwanjani.

Solskjaer kwa sasa amepokea kipigo mara mbili mfululizo kwenye Ligi Kuu England baada ya kutoka kupokea maumivu ya mabao 4-0 kutoka kwa Everton na kupokea maumivu ya kufungwa mabao 2-0 nyumbani mbele ya Manchester City.

Matokeo hayo yamemfanya akasirike na kuwavaa nyota wake wanne ambao anawalaumu kwa kushuka ghafla kiwango ndani ya kikosi hicho.

 Chris Smalling, Ashley Young, Nemanja Matic, Romelu Lukaku hawa ndio wapo kwenye mstari mwekundu wa kupigwa chini ili aanze kusuka kikosi kipya cha mauaji huku Paul Pogba ikiripotiwa kwamba amewaambia wachezaji wenzake anataka kusepa.

 Kocha huyo aliteuliwa kufundisha kwa muda timu hiyo, Desemba mwaka jana ambapo alipata matokeo mazuri mwanzoni na wachezaji kuonekana kujituma. Hata hivyo, upepo uligeuka ghafl a baada ya kupewa mkataba wa kudumu, Machi 28, mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic