April 25, 2019

MAUMIVU makubwa ambayo wameyapata watanzania kwa sasa huwezi kuzungumza kutokana na kutolewa kwa wawakilishi wetu wa timu ya Serengeti Boys kwenye mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya miaka 17 Afcon 2019.
Ni nafasi adimu ambayo tuliipata hasa kwa kuwa wenyewe tulikuwa wenyeji na kila kitu kilikuwa kinatuhusu sisi ila mwisho wa siku matokeo ambayo tunayapata ni ya kwetu kivyetuvyetu tofauti na wengine ambao ni wageni. 
Naona hasia za watanzania wengi wanamtupia zigo la lawama Kocha Mkuu wa Serengeti Boys Oscar Mirambo ila mimi naona hii sio sawa kwa sababu zigo analopewa Mirambo ni kubwa kuliko hata uwezo wake alionao hasa kwa kufundisha soka pamoja na ukubwa wa mashindano yenyewe.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilikuwa limepigwa ganzi kama halioni kinachoendelea hasa kutokana na maandalizi ambayo yalikuwa hasa tangu mwanzo kulikuwa kumepoa licha ya kuwakumbusha mara kwa mara mwisho wa siku matokeo haya tunayapata kile ambacho tulichopanda.
Kwa upande wa porojo hasa mipango yakuboresha benchi la ufundi ilikuwa ni hafifu maana mwanzo kulikuwa na mpango wa kuleta kocha wa kigeni mwenye uwezo wa kufundisha watoto na kutoka nje mwisho wa siku hakukuwa na kilichoendelea.
Kumwamini Mirambo na kumpa mashindano makubwa ambayo tulikuwa tunahitaji matokeo haikuwa sawa inaonesha ni namna gani TFF ilikuwa haijali na mwisho wa siku tunamwacha Mirambo ambaye hana uzoefu mkubwa anafanya kazi kubwa ambayo ipo nje ya uwezo wake.
Habari za kocha kutoka nje hata sijajua ziliishia wapi mwisho wa siku mashindano yanakuja bado hakuna jambo linalozungumziwa zaidi ya kuona kwamba tupo tayari ilihali kuna vitu vya msingi vya kufanyia kazi ili mambo yaweze kwenda sawa.
Ilibidi TFF wangetafuta kocha mwingine ambaye ana uwezo mkubwa na uzoefu kwenye mashindano ya kimataifa na sio mashindano ya kirafiki ambayo amekuwa akihusika kushiriki na kufikiri kwamba tayari ameiva kushindana kuna vitu vya msingi vya kufanya.
Haikuwa sahihi kumbebesha majukumu mazito peke yake ilibidi awe anasaidiwa na kocha mwenye uzoefu huku naye akipata uzoefu ndio maana matokeo yake amekuwa akifanya majaribio katika vitu vigumu ambavyo watanzania walikuwa wanahitaji matokeo.
Tumepoteza nafasi ya kipekee ambayo ni ngumu kuipata hasa kwa vijana hawa ambao msimu ujao hawatakuwepo tena hatua hii maana muda wao umekwisha ni lazima tuache kujuana na kufanya kazi kwa manufaa ya Taifa.
Tumeshindwa kuweka usiriazi kwenye mambo ya msingi na kuweka kwenye mambo mengine jambo ambalo limetughrimu moja kwa moja hii ni aibu na ni maumivu makubwa ambayo TFF hawana budi kuyabeba na kuyafanyia kazi.
Nadhani labda tungewekeza kwenye masuala ya ufundi tukaachana na masuala ya zawadi kwa watoto pamoja na fedha jambo ambalo liliwaharibu kisaikolojia watoto kuwaza mengine kabisa hali hii ni mbaya na ni msalaba mzito ambao tumewaachia watanzania hasa kwenye soka.
Hivyo kama kulikuwa kuna ulazima wa kuelekeza tungeanza na benchi la ufundi mambo mengine yangefuata
Tumepoteza fursa ya kwenda Brazili kwa kushindwa kuwa na malengo sahihi na mipango sahihi ni muda wa TFF kushtuka na kuanza kuweka mipango upya ili baadaye tutakapopata nafasi kama hizi zisiwe za kufanya majaribio matokeo yake yatatupoteza.
  
Kutoka Championi

4 COMMENTS:

  1. Umesema ukweli
    kabisa,viongozi wababaishaji tuu

    ReplyDelete
  2. Kim poulsen aliondoka kwa sababu gani wamejaa ubabaishaji tu

    ReplyDelete
  3. HUO NDIO UKWELI HALAFU WABISHI HAWAPOKEI USHAURI VISINGIZIO TUU MKIFUNGWA ETI OOH TUMEJIFUNZA MENGI SASA MAFUNZO YA ZAMANI ULIYOYAPATA UMESHINDWA NINI KUYATUMIA? KWAKWELI INAUMA SANA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic