April 21, 2019


KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kilichowaponza Simba jana ni kujiamini kupita kiasi hali iliyowapa nafasi ya kuwatungua mabao 2-0 haraka kipindi cha kwanza kabla ya kipindi cha pili kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Emmanuel Okwi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa alipania kuwanyoosha Simba kutokana na kasi yao kutafuta ubingwa huku wakisahau kwamba kuna timu ambazo zinapambana kubaki kwenye ligi.

"Niliwapanga wachezaji mapema na nikawaambia kwamba tupo kwenye kipindi kigumu cha mpito licha ya kuwa na uwezo tulikuwa tunachekwa na watu sikuwavunja moyo niliwaambia wanaweza na tukafanikiwa kushinda mbele ya Simba.

"Kama timu inacheza inapoteza kwangu haikuwa mbaya kwa kuwa nilikuwa naona sio mbaya tunauwezo wa kufanya kitu kikubwa, wapinzani wetu walikwa wanajiamini na walipania kubeba pointi tatu ambazo nasi tulikuwa tunazihitaji, hivyo kwa sasa bado tunapambana ili kubaki ligi kuu," amesmea Maxime.

1 COMMENTS:

  1. Mexime simba hao nyie ni mboga yenu ya kila siku hata msingejiandaa kihivo ila tyu msijemkachezesha mchezaji mwenye kadi 3 za njano hawakawii kuwahadaa mashabiki ooho tunaenda FIFA wakat siku hiz matokeo ya uwanjani hayahawahi badilishwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic