April 21, 2019


Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys, Oscar Mirambo amewaomba radhi Watanzania baada ya kuboronga kwenye michuano ya Afcon.

Serengeti Boys ambao ni wenyeji wa michuano hii wamepigwa chini bila kuambulai hata pointi moja kwenye mchezo mitatu ambayo walishuka uwanjani kupambana kuanzia ule wa ufunguzi na wa mwisho pale Taifa.


Kwenye kundi A wameruhusu kufungwa mabao 12 huku wao wakifunga sita na mawili wamefunga kwa penalti na wana pointi sufuri kwenye kundi A wakiwa wanaburuza mkia.

Mirambo amesema benchi la ufundi limejifunza mengi katika mashindano hayo na kuomba msamaha kwa kushindwa kuwapa kile ambacho walitarajia.

"Nilikuwa nahodha kwenye msafara mpaka meli inazama siwezi kukwepa lawama ni halali yangu katika hili ila haikuwa lengo langu na lengo la benchi la ufundi.


 "Tumeponzwa na imani yetu hasa baada ya kufanya maandalizi tukaamini yanatosha kumbe ilikuwa bado, tumejifunza kutokana na makosa tuna amini wakati mwingine tutafanya maajabu," amesema Mirambo.

6 COMMENTS:

  1. tujipange tena basi!
    lawama hasitatusaidia sasa!

    ReplyDelete
  2. Nadhan benchi la ufundi lingejiuzulu tu aisee. Kwani Shime TFF walimuacha wapi?

    ReplyDelete
  3. UPUUUUUZI MTUPU ONDOA BENCHI LOTE LA UFUNDI. WATU HAMSIKILIZI USHAURI MPAKA TUNAAIBIKA HIVYO.

    ReplyDelete
  4. WAKATI GANI MWINGINE? ONDOKENI. MMELIPA TAIFA AIBU KUBWA.

    ReplyDelete
  5. Beno: Tumefungwa magoli mepesi
    SUNDAY APRIL 21 2019




    Kwa ufupi
    Beno alisema pia hata kwa upande wa ushambuliaji wakati mwingine wamekuwa wakicheza kwa ubinafsi kutokana na kila mmoja kutaka kuonyesha uwezo wake badala ya kucheza timu kiujumla.
    ADVERTISEMENT
    By Thomas Ng’itu, Mwananchi tng’itu@mwananachi.co.tz
    Dar es Salaam. Kelele zimekuwa nyingi kwa namna ambavyo makipa wa Timu ya Taifa Tanzania chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ jinsi wanavyokuwa wanafungwa magoli ya kawaida, ishu hiyo imemfanya kipa wa timu ya Taifa Tanzania, Beno Kakolanya kufunguka namna makipa hao wanavyocheza.

    Kakolanya alisema amewafuatilia vijana hao lakini changamoto imeonekana kwa makipa.

    “Kweli makipa huwa tunafungwa lakini makipa wetu wamefungwa magoli mepesi sana.

    “Nafikiri wanatakiuwa walimu wao kuongeza juhudi ya kuwapa maelekezo kwani bado ni wadogo na pia ni wachezaji wazuri hivyo kuna vitu vikiongezwa kwao watakuwa kuwa tishio hapo baadae,”alisema.

    Beno alisema pia hata kwa upande wa ushambuliaji wakati mwingine wamekuwa wakicheza kwa ubinafsi kutokana na kila mmoja kutaka kuonyesha uwezo wake badala ya kucheza timu kiujumla.

    “Bado ni vijana wanazidi kukua polepole wanatakiwa waelekezwe namna ambavyo wanatakiwa wafanye kwenye mashindano kama haya.

    “Pamoja na kufanya ovyo, matokeo ndio kila kitu kwa timu halafu hilo la mmoja mmoja linakuja baadae,” alisema.

    ReplyDelete
  6. KOCHA HATUFAI AONDOKE NA BENCHI LOTE LA UFUNDI WAMTUPISHE WAKAE MBALI KABISA NA TIMU WAMETUTIA AIBU KUBWA HAWASIKILIZI USHAURI TULISEMA SANA KIPA HATOSHI WAO BADO TU WAMEMNGANGANIA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic