April 30, 2019


MGOMBEA wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dr Mshindo Msolla amesema kuwa uzoefu wake wa michezo kwa muda wa miaka 40 utamsaidia kuweza kutekeleza mipango ya klabu kwa wakati na hesabu zake ni kuirudisha timu kwa Wananchi.

Yanga inatarajia kufanya uchaguzi wake Mei 5 mwaka huu na leo kampeni zimezinduliwa rasmi kwa wagombea ili kupata viongozi wapya kwa ngazi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ndani ya Yanga.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo makao makuu ya Yanga, Msolla amesema kuwa amedhamiria kuleta mabadiliko ndani ya Yanga ili kutatua changamoto ya ombwe la uongozi ambalo lilikuwa linaathiri ufanisi wa klabu.

"Kwa kipindi kirefu kumekuwa na changamoto ya kiuongozi na matokeo yake changamoto hiyo imefanya kuwe na ombwe la uongozi, nimeamua kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa klabu kwa sababu nina uzoefu wa kutosha hasa baada ya kuwa kwenye tasnia ya mpira kwa muda wa miaka 40 katika nyanja mbalimbali.

"Nitahakikisha ninajenga umoja ndani ya klabu kwa wanachama na wapenzi wa Yanga na kuirudisha timu kwa wananchi kwa kuimarisha matawi yaliyopo, kuanzisha matawi mapya, matawi kupelekewa katiba ili wawe na uelewa wa katiba ya klabu yao na kuendeleza mchakato wa maboresho ya mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.

"Nitahakikisha Yanga inatengeneza Historia yake kwa kuboresha eneo la klabu na kufanya iwe sehemu ya utalii kama ulaya bila kusahau maboresho ya uwanja wa Kaunda pamoja na ukarabati wa jengo la klabu pamoja na kuweka misingi bora ya uwajibikaji," amesema Msolla na kuomba wanachama wamchague.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic