April 22, 2019


Nyota wa zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila, amewataka wanachama wa klabu hiyo kuwa makini katika kuchagua viongozi wapya kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Mei 5 mwaka huu.

Lunyamila ambaye aliwhai kutamba na kikosi cha Yanga miaka ya nyuma, ametoa tahadhari hiyo ili kuepusha utamaduni wa kupigiana kura wa kujuana.

Mkongwe huyo amefugunguka kwa kueleza kuwa Yanga inahitaji viongozi watakaoipa taswira nzuri klabu ili iepukane na wakati mgumu inaopitia hivi sasa.

Ameeleza inafikia hatua wanachama wawe makini wakati wa upigaji wa kura zao kwa kuchagua watu sahihi wenye uchu wenye maendeleo.

Tayari mchakato wa uchaguzi unaenda vizuri na huku wadau wengi wa klabu hiyo wakisubiria kwa hamu siku ya uchahuzi huo

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic