April 22, 2019


Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali amesema anatamani kuona tarehe 5 Mei inafika haraka ili uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ufanyike.

Yanga itafanya uchaguzi wake mkuu mei 5 ili kupata viongozi wake wapya ambao wataongoza kwa muda wa miaka minne ijayo.

Akilimali amesema amekuwa na uchu wa kuiona Yanga inafanikiwa kupata viongozi wapya kwani imekaa muda mrefu bila kuwa na uongozi.

Ameeleza anatamani tarehe 5 ifike haraka ili naye akapige kura yake kwani ni haki yake na amejinadi lazima akapige kwa kiongozi ambaye kwake anaamini ataleta mabadiliko Yanga.

Aidha, Akilimali amewataka wanachama wa Yanga kuhakikisha wanachagua kiongozi makini na mwenye sifa nzuri za kuiongoza klabu yao ili ifike mbali kimaendeleo.

4 COMMENTS:

  1. YANGA SIO KWAMBA HAIKUWA NA UONGOZI MBONA SHUGHULI ZETU ZA KILA SIKU ZIMEKUWA ZIKIFANYIKA ILA HATUKUWA NA SAFU YA VIONGOZI HALALI TULIOWACHAGUA KWENYE UCHAGUZI MKUU. SASA MEI 5 TUNACHAGUA FULL SQUAD HIYO NDIO DIRA MPYA YANGA OYEE

    ReplyDelete
  2. Mie ningewashauri tumchaguwe Mzee wetu Akilimali maana ana sifa zote za uongozi pia ni mtu mwenye uzoefu na mpenda maendeleo

    ReplyDelete
  3. hata mia hana uongozi anauwezea wap mzee simielewi huyu

    ReplyDelete
  4. kama anautaka uongozi vipi sasa hakuchukua form ya uchaguzi au yeye kazi zake ni kuharibu pale mambo yanapoenda sawa ???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic