April 6, 2019


KOCHA wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems juzi asubuhi pale kambini Sea Scape aliwaita wachezaji wake nakwenda kwenye ukumbi maalumu na kuwekewa baadhi ya picha za video za mechi za Mazembe. 

Baada ya kumaliza jioni wakaenda mazoezini pale Viwanja vya Gymkhana jijini Dar na kufanya kwa vitendo ili kuwadhibiti wapinzani wao huku Aussems akitumia ufundi wake katika kuwaelekeza namna ya kukabiliana na Mazembe.

Sasa Aussems jana amezungumza na Waandishi wa Habari na kusema; “Tumejipanga, nimewaona Mazembe namna wanavyocheza wakiwa ugenini na nyumbani hivyo nimejipanga kukabiliana nao na vijana wapo tayari kupambana.”

Naye Kocha Mkuu wa TP Mazembe, Mihayo Kazembe, alisema, mechi yao hiyo itakuwa ngumu kutokana na wapinzani wao kuwa na rekodi nzuri wanapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Kazembe alisema: “Mechi itakuwa ngumu sana, tazama Simba ambayo tangu imeanza michuano hii msimu huu mpaka sasa imeshinda mechi zake zote za nyumbani. Si timu ya kuibeza.”

“Tumejipanga kwa hilo, tutahakikisha tunapambana kuona hatupotezi mchezo huu ili iwe rahisi kuvuka tukienda nyumbani ingawa Simba wanaweza kushinda kutokana na rekodi yao.”

Naye nahodha wa kikosi hicho, Rainford Kalaba, alisema: “Hii ni mara yangu ya tatu nakutana na Simba, nilikutana nao mwaka 2011 katika mechi mbili za michuano hii, ninavyoiangalia Simba hii na ile ni timu mbili tofauti.

“Hii ya sasa ina wachezaji wengi wazuri kulinganisha na ya miaka ile ambayo staa alikuwa Mbwana Samatta. 

“Niseme tu kwamba, mchezaji ambaye anaweza kutusumbua ni Chama (Clatous), huyu namfahamu vizuri kwa sababu huwa nakutana naye timu ya taifa Zambia, ni mbunifu uwanja na ana kipaji cha hali ya juu kinachomuwezesha kuamua mchezo muda wowote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic