April 21, 2019


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Newcastle United Ayoze Perez inayonolewa na Kocha Mkuu, Rafael Benitez, jana alifanikiwa kufunga mabao matatu ‘Hat trick’ dhidi ya Southampton katika ushindi wa mabao 3-1.
Newcastle ambao walikuwa ni wenyeji wa mchezo huo walifanikiwa kupata ushindi na kuzidi kujiongezea nafasi ya kutokushuka daraja msimu huu baada ya kupanda nafasi mbili kutoka nafasi ya 15 mpaka nafasi ya 12 wakiwa na pointi 41.
Perez ambaye ni raia wa Hispania kama kawaida yake amekuwa mchezaji wa kufanya vizuri mechi za mwisho wa msimu, jana alifanikiwa kupiga Hat trick yake ya kwanza ndani ya Newscastle.  
Mchezo wake unaofuata wa Ligi ya England ni dhidi ya Brighton FC utakaopigwa Jumamosi ya Aprili 27.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic