NI PIGO TENA SIMBA, BEKI TEGEMEO NJE WIKI MBILI, KUIKOSA MAZEMBE
Inawezekana kabisa kuwa ni pigo kubwa kwa klabu ya Simba ambapo mchezaji wake kutoka Ivory Coast, Serges Wawa, atakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili.
Wawa aliumia katika mchezo wa mwisho Simba ilipocheza dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wawa ameeleza kuwa ameambiwa na daktari wake akae nje kwa wiki mbili bila kufanya mazoezi ya aina yoyote kutokana na aina ya majeraha aliyoyapata.
"Nimeshafanya vipimo vya afya na nimeambiwa nikae wiki mbili bila kufanya mazoezi.
"Nimeshafanya vipimo ambavyo vilionesha nyama za paja zimeachia hivyi nitasubiri tena mpaka baada ya wiki hizo kumalizika nitajua kama nitaanza mazoezi au nitaendelea kusubiri." amesema Wawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment