April 9, 2019


KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa  kwa sasa Simba wanachotakiwa kufanya ni kusahau yaliyopita kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe licha ya kushindwa kupata ushindi na badala yake waanze kujiaanda kwa mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Congo.

Simba ilishindwa kutumia vema Uwanja wa nyumbani kwenye mashindano hayo na kuruhusu suluhu ya bila kufungana wikiendi iliyopita.

"Wachezaji na mashabiki kwa sasa hesabu za kukumbuka machungu ya kushindwa kushinda wayasahau bali waongeze nguvu kwenye maandalizi ya mchezo wao wa marudio utakaopigwa nchini Congo.

"Kushindwa kupata ushindi ni sehemu ya matokeo ambayo yanatakiwa yapokelewe na wachezaji, viongozi pamoja na mashabiki hivyo kufikiria matokeo yaliyopita kutawafanya washindwe kufanya vema mchezo wao ujao, hesabu zao kwa sasa ziwe ni mchezo wao wa marudio, wapambane wakapate matokeo, inawezekana kwenye soka," amesema Matola.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic