YONDANI ATEMWA NA ZAHERA CCM KIRUMBA MWANZA
Beki mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani, hajawa sehemu ya mazoezi ya leo asubuhi na kikosi cha Yanga kutokana baada ya kuumia katika mchezo wa jana dhidi ya African Lyon.
Mchezaji huyo ameshinda kujifua kuelekea mchezo wa Alhamis ya wiki hii ambapo Yanga itakuwa inachezA dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu bara.
Kikosi cha Yanga kitakuwa na kibarua hicho kesho kutwa mechi itakayokuwa ya 31 kwao kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa Kocha, Mwinyi Zahera, amesema kuwa mazoezi yanaenda vizuri na hakuna watakachokuwa wanakitafuta uwanjani zaidi ya alama tatu pekee.
Mpaka sasa Yanga ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 71 baada ya kucheza mechi 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment