SIMBA YAIAIBISHA YANGA KWA MAPATO MWANZA
UKISIKIA kipyenga kimelia ndani ya CCM Kirumba leo jioni, Simba itakuwa imeshatibua mambo kwenye maskani hiyo ya Yanga. Simba itakipiga na KMC kwenye mechi ya ligi katika Uwanja huo, hiyo ikiwa ni mechi ya tatu ya Mnyama ya ligi kwenye nyasi hizo msimu huu.
Sasa basi, takwimu za mapato kwenye mechi za ligi za hivikaribuni katika uwanja huo ambao Yanga inautumia kama nyumbani, ziko vizuri kwa Simba.
Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika ndani ya Chama cha Soka cha Mwanza, Simba kwenye mechi zake mbili tu dhidi ya Mbao na Alliance imeingiza Sh.96.6 dhidi ya 119.1 walizoingiza Yanga kwenye mechi tano.
Hiyo inamaanisha kwamba, Yanga ikiingiza na mapato ya leo dhidi ya KMC itawafunika Yanga kwani makadirio yanaonyesha mapato yake kwenye uwanja huo si chini ya Sh.Mil 40.
Kwenye mechi na Alliance waliingiza Sh.Mil 45.8 na Mbao Sh.Mil 50.7. Mechi ya Yanga; dhidi ya Kagera Sh.Mil 9.8,
Lyon Sh.Mil 7.9, Alliance Sh.Mil 38.3, Alliance Sh.Mil 27.2 na ule wa Mbao Sh.Mil 36. Hiyo ni rekodi kubwa ya mapato kwa Simba kutokea kwenye Uwanja huo katika misimu ya hivikaribuni haswa Yanga ikiutumia kama maskani yake na Uwanja wa Nyumbani. Tathmini ya Spoti Xtra imebaini kwamba Simba iliizidi Yanga kwa mashabiki kutokana na kufanya vizuri kimataifa.
CHANZO: SPOTI XTRA
Halafu wanadai wana mashabiki!Uharo mtupu .Yimu ulivyo na mashabiki popote inapocheza ni Simba .Takwimu hazidanganyina pia mapato ni ushahidi.
ReplyDeleteyanga ni wengi ila iman na timu yao hakuna, simba wanaenda kwa kuwa wana matokeo kabla ya mechi, hamkumckia mtangazaji wa azam kwny game ya kagera na simba pale kagera walipopga goli la pili alisema ni maajabu, it means hata media znajua simba anaenda kushinda
ReplyDeleteSio media tu hata kagera wenyewe hawaamini mpaka leo .Yanga walisherehekea kufugwa goli moja. Kikosi bora siku zote ndio kinachotabiliwa kushinda tuache kuongozwa na ushabiki wa kipuuzi. Timu imetoka robo fainali klabu bingwa sio timu ya Michezo ni timu nzuri.
ReplyDelete