April 26, 2019


BAADA ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys kufungashiwa mabegi na wapinzani wao Angola kwa kukubali kichapo cha mabao 4-2 sasa wameanza kazi ya kujiaanda kwa ajili ya wakati mwingine.
Serengeti Boys ilitakiwa ishinde mechi mbili tu kisha wachezaji kukwea pipa kwenda Brazil kushiriki kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17 mwaka huu ila mambo yakawa magumu kwao.
Kocha wa makipa, Peter Manyika amesema kuwa wanatambua maumivu waliyonayo watanzania ila haikuwa mipango yao kuvurunda kwenye michuano hii inayoendela jiji Dar.
"Haikuwa kwenye hesabu zetu ni matokeo mabaya kwetu na Taifa kiujumla ila hamna namna kwa kuwa hatuwezi kubadili matokeo ambayo yametokea hivyo kwa sasa ni kuanza mipango kwa ajili ya wakati mwingine," amesema Manyika
Serengeti Boys ambao ni wenyeji kwa sasa watakuwa ni mashabiki wakitazama namna wageni wakipeta kwenye ardhi ya nyumbani, huku wao wakiwa wameyaaga mashindano bila kushinda hata mchezo mmoja wala sare katika kundi A ambalo walimaliza wakiwa nafasi ya nne.
Kesho itachezwa fainali ya kwanza kumtafuta mshindi wa tatu kati ya Nigeria na Angola na Jumapili itachezwa fainali kati ya Guinea na Cameroon Uwanja wa Taifa na mechi zote ni saa 10:00 Jioni.



2 COMMENTS:

  1. Peter Manyika ndiye Kocha wa Makipa? Kipa wetu wa vijana hakuwa sawa hata kidogo na Indio sabbat mojawapo Mkubwa ya timu yetu kutolewa na kufungwa mechi zote 3. Lipo tatizo Mkubwa kwenye goal keeping.

    ReplyDelete
  2. Mpira kocha bwana asikwambie mtu hayo mengine yote mashongosho. Unawaona Liverpool walikuwa wa kawaida lakini yule Mjerumani kocha bana. Unaiona Man city licha ya utajiri waliokuwa nao walikuwa wanahangaika tu mpaka alipotua guardiola sasa wanatetema tu.Mifano ipo mingi yakwamba mpira unategemea uwezo wa kocha katika kazi yake . Serengeti boys kocha wake hakuwa na kiwango cha kuwawezesha vijana wale kushindana na vigogo vya soka Africa wenye kujua utamu wa kuwa expose vijana wao kupitia Afcon. Serengeti boys walionesha kuwa hawakuwa tayari kwa Afcon mapema tu walipokwenda Uturuki na kupata vipigo vya aibu na kama mabadiliko yalikuwa yafanywe pale ili kuikoa serengeti boys lakini kawaida ya watanzania huwa hatufikirii kumtibu mgonjwa mpaka tumuone anakufa. Baada ya ushiriki wa aibu Serengeti boys Afcon utashangaa kwanini kocha au benchi la ufundi wanashindwa kuwajibika? Ni Tanzania pekee kocha anaboronga anapewa kazi muhimu zaidi ya ile.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic