April 26, 2019


KIKOSI cha Yanga Princess kilicho chini ya kocha Mohamed Hussen 'Chinga' msimu huu baada ya kupanda daraja na kushiriki ligi ya wanawake inayodhaminiwa na kinywaji cha Serengeti kimepigwa nje ndani na wapinzani wao Simba Queens.
Simba Queens ambayo ipo chini ya kocha Mussa Mgosi ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Simba wamekuwa wababe msimu huu wa kwanza kwa Yanga wakiikaribisha kwa vipigo vikali.
Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa uwanja wa Karume, Simba Queens waliipiga Yanga Princess kwa jumla ya mabao 7-0 hali ambayo iliwafanya wawe wanyonge kwa muda wakati wa kutoka uwanjani.
Mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa uwanja wa Karume, Simba Queens waliipiga Yanga Princess mabao 5-1 na mzunguko huu Yanga Princess walijitutumua kupata bao na kupunguza idadi ya mabao.
Hivyo jumla Yanga Princess wameipa Simba Queens pointi zote sita na kukubali kupewa zigo la mabao 12 huku la kufutia machozi kwao likiwa moja tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic