BAADA ya kikosi cha Serengeti Boys kutolewa kwenye michuano ya Afcon inayoendela leo uwanja wa Taifa wamepishana na waamuzi wa nyongeza ambao wameongezwa.
Shirikisho la Soka barani Afrika Caf limetangaza kuongeza waamuzi wasaidizi wa nyongeza ‘Additional Assistant Referees’ (AAR) kwenye michezo ya nusu fainali ya michuano ya Afrika kwa vijana inayoendelea nchini.
Waamuzi hao wa nyongeza watakuwa wawili na watasimama pembezoni/nyuma ya magoli lengo likiwa ni kusaidia maamuzi ya matukio yoyote yanayoweza kutokea ndani ya eneo la penati kwa mujibu wa sheria za soka.
Mechi mbili za nusu fainali ya michuano hiyo zinapigwa leo Uwanja wa Taifa Dar es Salaam itakuwa kati ya Nigeria dhidi ya Guinea saa 10:00 jioni na Cameroon dhidi ya Angola saa 1:30 Usiku.
0 COMMENTS:
Post a Comment