April 24, 2019


BAADA ya kuishi kwa miaka kadhaa bila maelewano wala uhusiano, hatimaye msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, amepatana na baba yake mzazi mzee Abdul Juma ambapo jana mzee huyo aliibuka kwenye studio za Wasafi FM na kukutana na mwanaye.

Hilo limetokea jana usiku wakati Diamond akifanya mahojiano na kituo chake cha Radio cha Wasafi FM kuhusu maisha yake na vitu vingine anavyofanya kuhusu kazi zake za muziki.

Katika video iliyorekodiwa studio hapo inamwonyesha mzee Abdul akiingia studio ya Wasafi FM na kukutana na mwanaye Diamond ambapo walikumbatiana na kuketi kisha yakaanza mazungumzo ambapo baadaye waliamka na kucheza pamoja.

Akizungumzia tukio hilo, mzee Abdul amesema anajisikia faraja sana kupokelewa na mwanaye kipenzi hivyo faraja na furaha yake imerejea kuona mahusiano yao yamekuwa mazuri sasa huku akidai hali iliyokuwepo mwanzo ya kutoelewana ilikuwa ikimpa wakati mgumu.

“Mimi ni mtu mzima huyu ni mwanangu siwezi kumuomba msamaha, nataka tu haya yaishe,” amesema mzee Abdul.

Aidha, mashabiki wamempongeza Diamond kwa uamuzi huo wa busara wa kurejesha mapenzi kwa baba yake, na kumtaka sasa afungue ukurasa mpya wa mahusiano mazuri na wazazi wake wote wawili kwani hata kama wana mapungufu lakini ndiyo waliomleta duniani na kufanikisha maisha aliyo nayo sasa.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic