BEKI wa Simba, Pascal Wawa ambaye ataukosa mchezo wa leo dhidi ya TP Mazembe kutokana na kusumbuliwa na majeraha amesema kuwa anaiona Simba ikipata matokeo mbele ya wapinzani wao.
Wawa ambaye alipata majanga hayo walipocheza na Mazembe uwanja wa Taifa, amesema kuwa anaamini wachezaji watapambana na kupata matokeo yatakayoishangaza Dunia.
"Najua kwamba leo wachezaji wenzangu watakuwa na kazi ngumu kupambana mbele ya Mazembe ila nina imani watashinda na kusonga mbele kwenye michuano hii mikubwa Afrika.
"Kila hatua ipo tofauti na ushindani ni mkubwa nimewaona wachezaji wenzangu wana morali kubwa na wapo tayari kupambana hivyo mashabiki wasiwe na hofu wataishangaza dunia na Mungu atawasaidia na kuwalinda pia," amesema Wawa.
Kweli tumeshangaa sie walimwengu
ReplyDelete