April 13, 2019


UNAWEZA kusema rasmi kamati ya uhamasishaji wa kuichangia Yanga, iliyozinduliwa Aprili 6, mwaka huu ndani ya Morena Hoteli mjini Dodoma, ambayo iko chini ya Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, imeeleweka ambapo Watanzania waishio nchi za Marekani, Dubai na Uingereza wameichangia Sh bilioni moja.

Michango hiyo inajumuisha Watanzania wanaotoka katika nchi nane maarufu kama Diaspora ambazo kwa pamoja zimeunda group la WhatsApp na kuipokea kwa kishindo kampeni hiyo, kiasi cha kuhamasishana mara moja na kuanza michango ambayo hadi sasa inadaiwa kukusanya zaidi ya kiasi hicho.

Katibu wa Kamati ya Uchangiaji ya Yanga, mhandisi Deo Mutta, alisema mara baada ya kuizindua rasmi kampeni hiyo, Jumatatu iliyopita aliunganishwa katika group la Watanzania hao na kumpatia mikakati yao huku wakiomba akaunti rasmi watakayotuma fedha za mchango wao.

“Kwa makadirio ya haraka hadi sasa hivi nimeona takribani dola mia tano na zaidi zimeshachangwa kupitia group hilo, na nchi ambazo zimo ni pamoja na Marekani, Saudia, Uingereza, Uturuki, Sweden na Dubai na hizi ni kati ya nchi nane ambazo ninaziona katika group hilo, lakini kwa hamasa ambayo wanayo bado wanazidi kuhamasishana hata katika nchi nyingine zaidi ili zijiunge katika kampeni hiyo.

“Ni matumaini yangu kampeni hii inaonyesha mafanikio makubwa na kwamba siku si nyingi tutavunja lengo kwani hata lengo la kwanza katika uzinduzi wetu wa Dodoma tulilivuka, tulipanga kuanza kuchangisha katika uzinduzi huo Sh milioni 300 lakini siku hiyo kupitia ahadi tuliļ¬ kisha Sh milioni 600 na kitu,” alisema Mutta.

10 COMMENTS:

  1. Dollar Mia 500 in million Mojave’s na laki 1. Wewe billion unapata kwa exchange rate ipi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. hayo ni makosa ya kawaida ktk uandishi.....tumia akili bro,sio unailaza akili ukisubiri kutafuniwa.

      Delete
  2. Aisee wahandishi was kibongo laana sana

    ReplyDelete
  3. Bilioni kwa rate ya Zimbabwe .Zimechangwa dola 500 imekuwa kelele.

    ReplyDelete
  4. Uandishi wenu ni ovyo maana una kengo la kukwamisha zoezi wewe saleh na crew yako

    ReplyDelete
  5. mnapotosha sana vijana wetu wanaoamini kila kinachoandikwa na waandishi ni sahihi dola mia tano inaweza kuwa sawa na shilingi bilioni moja?

    ReplyDelete
  6. Waandish hawa wa blog hii hawapo serious na kazi yao na hawajitambui kabisa

    ReplyDelete
  7. Hivi kwa nini uncle Magu haingii na huku kupambana na hawa waandishi vilaza?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic