April 9, 2019


Tetesi za soka barani ulaya leo Jumanne hizi hapa

Man United kutoa pauni milioni 50 kwa Rice

Manchester United wanatajwa kutangaza dau la usajili la pauni milioni 50 ili kumnasa kiungo kinda wa West Ham Declan Rice, 20. (Irish Independent)

Rice, amesema kujiunga na West Ham ulikuwa uamuzi bora kabisa aliowahi kuufanya baada ya Chelsea kumtema akiwa na miaka 14. (Standard)

Tagliafico kutua Uingereza, Arsenal watajwa

Beki wa kushoto wa Ajax Nicolas Tagliafico, 26, amesema kuwa mwisho wa msimu huu utakuwa ni muda muafaka wa kuhamia kwenye Ligi ya Uingereza. Beki huyo raia wa Argentina anawindwa na Arsenal. (Mirror)

Msaidizi wa Ole amtaka Pogba kusalia United

Kocha msaidizi wa Manchester United Mike Phelan amesema kiungo wa klabu hiyo Paul Pogba, 26, bado hajamaliza kazi yake na anamtaka mchezaji huyo kusalia Old Trafford. (Telegraph)

France Football wamtaka Pogba kuondoka United

Jarida la 'France Football' la nchini Ufaransa linamshawishi Pogba kuhama Old Trafford na kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu. (France Football - in French)

Rais Barcelona asema walimshindwa Pogba sababu ya dau kubwa
Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amesema klabu yake ilitaka kumsajili Pogba kutokea Juventus lakini ilishindwa kufikia dau la United mwaka 2016. (ESPN)

Everton kutangaza dau la usajili kwa Adams

Everton wanajiandaa kutangaza dau la usajili ili kumnasa mshambuliaji wa Birmingham City Che Adams, 22. (Football Insider)

West Ham kutompatia mkataba mpya Caroll

West Ham hawatampatia Andy Carroll, 30, mkataba mpya mwishoni mwa msimu. Mshambuliaji huyo amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu, hali inayomfanya kushindwa kurejea dimbani mpaka msimu utakapokwisha. (Mail)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic