April 30, 2019

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00.

Simba itashuka kwa mara ya kwanza uwanja wa Uhuru msimu huu ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-0 mchezo wa kwanza mbele ya JKT uliochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.

"Kazi kubwa kwa sasa ni kuona tunapata matokeo chanya mbele ya wapinzani wetu, tunawaheshimu na tunajua ushindani ulivyo ila hakuna namna lazima tupambane.

"Ushindani kwa sasa kwenye ligi ni mkubwa na kila timu ni bora ninaamini wachezaji wangu watapambana, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema Aussems.

1 COMMENTS:

  1. Wakati huu hakuna timu ndogo hasa ukizingatia ligi ipo kwenye lala salama na wachezaji pia wa timu pinzani wanataka kuonekana. Hakuna budi Simba kila mechi fainali kwa sasa kwani dharau ya aina yeyote ile ni sawa na mtu anaekwenda kukichapa kilevi wakati akimfukuza mwizi aliekaribia kumshika. Yanga wapo tayari kufanya lolote hata ushirikina kuhakikisha viporo vya Simba havi liki. Kwa Simba dawa ya kukata kidomodomo cha Zahera na Yanga ni wachezaji kujitoa na kuhakikisha wanashinda kila mechi na hilo linawezekana kwa viwango vya timu za ligi kuu kama kweli wachezaji na benchi la ufundi la Simba watakuwa siriaz sio kujifanya usupa star wa kwenye magazeti tu. Kila la kheri Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic