April 30, 2019


Timu ya Yanga imeweka rekodi ya aina yake pengine tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Bara kuanzishwa hapa nchi kwa kuja na aina ya jezi tofauti tena ikicheza dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo, Yanga ilikuja ikiwa na jezi zingine mpya, jezi ambayo imekuwa ni ya tisa sasa kwa timu hiyo kutoka mitaa ya Twiga, Jangwani kwa msimu huu.

Katika mchezo huo ilioshinda kwa bao 1-0, Yanga ilikuja na jezi aina mpya zenye rangi ya njano na michirizi ya kijani na kuwaSAPRAIZI wanachama na mashabiki wake uwanjani.

Hivi karibuni Kaimu Katibu Mkuu wa timu hiyo, Omar Kaya, aliwahi kunukuliwa akisema kuwa wanabadilisha jezi kwasababu wanaamua kama uongozi na hakuna atakayeweza kuwangia cha kufanya.

Mabadiliko hayo ya jezi yamekuwa yakiwakera baadhi ya mashabiki kutokana na kubadilishwa mara kwa mara na kushindwa kujulikana ni jezi ipi rasmi inayotumika ikiwemo ya nyumbani na ugenini.

Aidha, wapo pia ambao wamekuwa wakipongeza wakieleza kuvutiwa na jezi hizo ambazo Yanga imekuwa ikibadilisha kila wakati.

5 COMMENTS:

  1. alimradi ina nemb ya wadhamini lakini uwkeli tuuseme, kwanza duniani kote timu hutambulisha jezi rasmi ya nyumbani na ugenini kabla ya ligi kuanza na hii inatoa fursa pia kwa soko la jezi kwa washabki, pili moja ya eneo ambalo timu zinakosa mapato na kulia njaa ni uuzwaji wa jezi kiholela, timu kama yanga yenye mashabiki lukuki ingeweka utaraibu maalum wa kuuza jezi yake rasmi ni mapato makubwa sana...tuendelee kulia njaa ilihali uchumi tumeukalia

    ReplyDelete
  2. Baadhi ya Vyura wanashangilia mijezi tofauti kila uchao wakifikiri wanaikomoa Simba, kumbe wanajikomoa wenyewe. Na safari hii mmeamua kuja na jezi KHANGA moko sijui tuseme MADELA. Hizo jezi ni kanga kabisa.
    Washabiki wa Yanga wanaoshadadia hizi jezi tofauti tofauti hawana habari kuwa dizaina wa hiyo mijezi Dismas10 na kwamba yeye anapata chake kwa kila design ya jezi. Anaendelea kujinufaisha yeye kwa mgongo wa Yanga. Anaiumiza Yanga kwa kuikosesha mapato ya jezi. Katika mazingira haya klabu itauzaje jezi?
    Uongozi wa klabu unawaambia hakuna kati yenu wa kuwapangia cha kufanya, na bado kuna vyura mnashangilia tu, na mabakuli mnajaza wakati chanzo cha mapato ya klabu kinachezewa hivi.
    Vyura kazi mnayo

    ReplyDelete
  3. Halafu wanatembeza kopo!hela ya jezi wakalipe deni

    ReplyDelete
  4. Jezi ya Tisa yanga duuh mganga wao kawadanganya sana

    ReplyDelete
  5. usiseme neno bila ushahidi kama binaadam hawatokufanya kitu yupo muumba wa kila kitu atapitisha hukumu yake , chunga sana kumtuhumu mtu bila ya kuwa na ushahidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic