April 26, 2019



Kocha Mkuu wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer amesema ataendelea kumtumia kipa wake namba moja, David De Gea licha ya kuandamwa na makosa mfululizo.


 Solskjaer amesema anaamini De Gea ni mmoja wachezaji bora na wana msaada mkubwa katika kikosi chake.

"Hali ya makosa hutokea, ninaamini David atarejea na mechi dhidi ya Chelsea matanza," ámesema Solskjaer.

Kwa miezi miwili sasa De Gea ameshindwa kucheza hata mechi moja bila ya kuruhusu nyavu zake kutikiswa.

Mbali na hiyo, kipa huyo raia wa Hispania ameandika rekodi ya kuwa kipa wa kwanza wa Manchester United kufungwa mabao 50 katika msimu mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic