April 3, 2019


KIKOSI cha Yanga leo kimefanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao wa kesho dhidi ya Ndanda FC utakaochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera itashuka kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Zahera amesema kuwa hana mashaka na kikosi chake kwani tayari amewapa mbinu mpya zitakazowasaidia kupata matokeo chanya kwani hesabu zao ni kupata pointi tatu.

"Tumefanya mazoezi kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wetu, naamini kwa namna nilivyoandaa kikosi tutapata matokeo kwani uwezo wa kushinda upo mikononi mwetu, mashabiki watupe sapoti," amesema Zahera.

Yanga imecheza michezo 28 kwa sasa ikiwa imejikita kileleni na pointi zake 67.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic