April 6, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera leo asubuhi anatarajiwa kusafi ri kwa ndege kwenda mkoani Dodoma.

Mkongomani huyo atasafi ri mkoani humo kwa ajili ya uzinduzi wa Kamati Mpya ya Uhamasishaji wa Michango ya Yanga ilivyokuwa chini ya Waziri na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.

Kamati hiyo tayari ilikuwa ishaanza kampeni yake ya uhamasishaji wa kukusanya fedha hizo ambazo ni shilingi bilioni 1.5 zitakazotumika kwa ajili ya usajili msimu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi na kuthibitisha na Ofisa Habari Msaidizi wa Yanga, Godlisten Anderson ‘Chicharito’ kocha huyo anatarajiwa kusafiri kesho (leo) kwa ndege.

Anderson alisema, kocha tayari wamemkatia tiketi ya kwenda Dodoma na kwenda Mwanza kuungana na timu itakapokuwa Uwanja wa CCM Kirumba itakapovaana na African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Jumatatu.

“Kamati ya Uhamasishaji Mpya iliyochaguliwa hivi karibuni kesho (leo) itazinduliwa rasmi huko Dodoma. “Katika uzinduzi huo Kocha Zahera anatarajiwa kuwepo kwa lengo kuongeza hamasa katika uzinduzi huo.

“Baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo siku hiyo ya Jumamosi haraka atachukua ndege na kuungana na wachezaji kambini kwa ajili ya mchezo na Lyon,” alisema Anderson.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic