May 12, 2019


KUELEKEA kwenye mchezo wa leo wa Ligi Kuu England kati ya Arsenal na Burney utakaopigwa uwanja wa Turf Moor, meneja wa Arsenal, Unai Emery amesema kuwa wachezaji wake wana hasira na njaa ya kufunga mabao.
Emery amesema kuwa ametumia muda mwingi kuwatazama wapinzani wake hali ambayo inamfanya aamini ataibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa leo.
"Ninakwenda kwenye mchezo mgumu nikiwa najua kwamba wachezaji wangu wana hasira na shauku ya kushinda mchezo wetu kwa nama yoyote ile.
"Ninakumbuka mchezo wa mwisho kwa wapinzani wangu niliutazama ilikuwa dhidi ya Chelsea na walitoka sare ulikuwa mchezo mgumu na ninatambua hata kwangu pia utakuwa mgumu, mbinu zao ni mipira mirefu na wanapiga pasi nyingi hivyo nimejipanga kwa kila namna," amesema.
Arsenal ipo nafasi ya 5 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 37 imejikusanyia jumla ya pointi 67.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic