KUELEKEA mchezo wa kesho wa fainali ya kombe la Shirikisho 'FA' makocha wa timu zote mbili wamesema kuwa vikosi vyao vipo tayari kutwaa ubingwa ndani ya dakika 90 uwanja wa Ilulu, Lindi.
Lipuli FC kesho itamenyana na Azam FC kwenye fainali ya kombe la FA ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana kwenye fainali ya kombe hili.
Kocha wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wanaiheshimu timu ya Lipuli ila wamejipanga kufanya vizuri kwenye fainali.
"Kama timu imefika fainali na imewatoa vigogo sio timu ya kubeza, hata sisi pia tunalitambua hilo ila hamna namna kesho lazima tuingie kwa tahadhari kwenye kazi tutakayokwenda kuifanya, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema Cheche.
Kocha wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa wamejipanga sawasawa kufanya vizuri kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya.
"Tumefanya maandalizi kwenye mazingira magumu lakini tumejipanga kushinda, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti nina imani tutafanya vema," amesema Matola.

0 COMMENTS:
Post a Comment