May 24, 2019


BAADA ya Azam FC kupoteza mchezo wa kwanza mbele ya Yanga uliochezwa uwanja wa Uhuru sasa hesabu kali za kocha wa Azam FC Idd Cheche ni kulipa kisasi kwa wapinzani wake hao ambao atafunga nao ligi msimu huu.

Azam FC itamenyana na Yanga, Mei 28 uwanja wa Uhuru ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kufungwa kwa mara ya kwanza na mchezaji wao wa zamani Mrisho Ngassa bao 1-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa makosa ya mwanzo wameyagundua hivyo itakuwa ngumu kupoteza tena mchezo wao wa marudio.

"Kwa mwalimu yoyote duniani lazima aangalie namna bora ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa pili, kama wa kwanza tulipoteza ni muda wetu kulipa na kubeba pointi tatu.

"Hakuna kingine tunachokitafuta kwa kuwa nafasi ya kwanza na ya pili msimu huu sio zetu ila haimananishi mchezo wetu wa mwisho tusiupe kipaumbele hapana lazima tupambane," amesema Cheche.

Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa imecheza jumla ya michezo 37 imejikusanyia pointi 72 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic