May 24, 2019

NYOTA wa Mwadui FC, Salim Aiyee amesema kuwa kwa sasa akili zake amewekeza kwenye suala zima la kupambana na timu yake isishuke daraja kabla ya kuamua kusaini Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

Aiyee ambaye ni kiboko ya John Bocco na Emmanuel Okwi wote wa Simba akiwa ametupia jumla ya mabao 17  huku Okwi akiwa ametupa mabao 15 na Bocco akiwa nayo 17 anawindwa na timu nyibgi bongo ikiwa ni pamoja na Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aiyee amesema kuwa kwa sasa hana presha na suala la kujiunga na timu yoyote bongo kwani amekuwa akiwasiliana na viongozi wengi wakihitaji saini yake na yeye ana majukumu mengine kwa sasa.

"Timu yangu ya Mwadui ipo na kazi kubwa kwa sasa kuona namna gani itabaki kwenye ligi msimu ujao hivyo nimewaambia viongozi wote wasubiri kwanza wasinipe shinikizo la kusaini kwa sasa.

"Nimeongea na baadhi ya viongozi wa timu ya Yanga ila siwezi kuwataja kwa sasa pamoja na timu nyingine wamekuwa wakiuliza juu ya mkataba wangu wote nimewaambia wasubiri baada ya Mei 28 nitawapa majibu," amesema Aiyee.

Mchezo wa mwisho Mwadui ambayo ipo nafasi ya 18 ikiwa imecheza michezo 37 na ina pointi 41 itamenyana na Ndanda FC ambayo ipo nafasi ya 7 imecheza michezo 37 na ina pointi 48.

Kwa upande wa uongozi wa Yanga, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kuwa suala la usajili kwa sasa ameachiwa kocha Mkuu, Mwinyi Zahera yeye ndiye mwenye maamuzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic