May 1, 2019


Baada ya kikosi cha Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika dakika za mwisho jana dhidi ya JKT Tanzania, gumzo kubwa ni kuhusiana na dakika saba za mwisho zilizoongezwa na Mwamuzi wa mchezo huo.

Simba iliibuka na ushindi huo kupitia bao la Hassan Dilunga aliyefunga katika dakika ya mwisho kabisa zikiwa zimeongezwa hizo saba ambao zimeleta hoja kubwa haswa kwa mashabiki wa upande wa pili ambao ni Yanga.

Kupitia mitandao na hata vijiweni kumeonekana mashabiki wengi wa Yanga wakihoji imekuwaje mechi hiyo iongezewe dakika saba na wengi wao wakiamini hazikuwa zinastahili.

Asilimia kubwa wamesema kuwa ni kama kulikuwa na upendeleo wa kuitafutia Simba matokeo wakiamini mechi ilikuwa inamalizika kwa matokeo ya 0-0.

Malalamiko hayo yamekuja ikiwa Simba na Yanga zinawania ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku wekundu hao wa Msimbazi wakiwa bado na viporo vya mechi wakielekea kuvikamilisha.

7 COMMENTS:

  1. Kwani nyie wananchi hamjui?zilipangwa dakika 120 halafu penalti zingefuatia

    ReplyDelete
  2. mbona za Lipuli hamzizungumzii?

    ReplyDelete
  3. Kawaida ya mfa maji haachi kutapa tapa

    ReplyDelete
  4. Dakika 9 za Lipuli mbona hamzitaji?Kufeli huwa kunatafutiwa sababu nyingi.Ziliongezwa dakika 7 kwa JKT kupoteza muda.Jana mechi ya Totenham nä Ajax kuiongezea dakika 5 kipindi cha kwanza na dakika 4 kipindi cha pili.Au hapo aliyebebwa nani?Imekuwa tabia ya wapenzi wa Yanga kutafuta kichaka cha kulalamika kwenye kila kitu.

    ReplyDelete
  5. Wamesahau mechi ya Lipuli walipewa dak 7 za nyongeza. Walifungwa mapema na wakashindwa kutumia muda huo !Kukiwa na substitition kila moja huchukua wastani wa dak moja!muda husimamishwa na kuhesabiwa!Jana substitution zote zinazoruhusiwa kutumika zilitumika. Na mpira unaposimama kama mchezaji ameumia muda husimamishwa. JKT walikuwa wanacheza rafu za kuumiza.. Na kipa wao mara ngapi aliumia?Kama aliumia kweli!Kujiumiza na kuumiza kwao kuliwaponza.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic