May 1, 2019


Baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga wamelitupia lawama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuipangia Simba kucheza na Sevilla ya Spain.

Hatua hiyo imekuja mara baaa ya TFF kuthibitisha kuwa Simba itakipiga na Sevila kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa kirafiki kuelekea msimu ujao.

Mashabiki na wanachama hao wamesema kuwa awali ilielezwa kulipaswa kufanyike mechi baina ya watani wa jadi ili mshindi ndiyo acheze na Sevilla.

TFF kwa kushirikiana na SportPesa wameamua kuwachagua Simba kucheza na Sevilla kwa kuangalia ubora wa miaka ya hivi karibuni.

Rekodi zinaonesha kuwa Simba ndiyo wamekuwa bora zaidi katika Ligi Kuu Bara kwa miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na timu zingine.

1 COMMENTS:

  1. Walipeleka kikosu cha pili eti kikosi cha kwanza kilihitaji mapumziko..na kujiandaa FA cup. ligi kuu na Sport pesa...matokeo yake Zanzibar hawakufika mabali, Sport pesa wakaharibu kabisa.Labda kama wamebetia FA cup.. Kwani na ubingwa wasahau.. imebaki kulalamika kila kitu kama mama mjamzito...tumieni ndimu!mara penalt, mara dak 7 utadhani kule kwa Lipuli zilipoongezwa 9 alicheza Lipuli pekee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic