NAHODHA wa Yanga, Ibrahim Ajibu ameendelea kutakata kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, mpaka sasa akiwa ni kinara wa kutupia pasi za mwisho ndani ya Yanga pamoja na Ligi Kuu Bara Tanzania.
Ajibu leo amefikisha pasi yake ya 17 wakati akitimiza majukumu yake mbele ya Tanzania Prison na kuifanya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru.
Pasi ya Ajibu aliitoa kipindi cha kwanza na ikamaliziwa na kiungo, Pappy Tshishimbi dakika ya 23 kupitia mpira wa faulo aliupiga kiungo huyo.
Ajibu amefunga mabao 6 mpaka sasa na amehusika kwenye mabao 17 ya Yanga kati ya mabao 54 waliyofunga na kufanya ahusike kwenye jumla ya mabao 23.
Ushindi wa leo unaifanya Yanga kujikita kileleni ikiwa na pointi 80 baada ya kucheza michezo 34 amebakiza michezo minne kumaliza mzunguko wa pili.
Hii ni pasi yake ya pili mfululizo kwenye Uwanja wa Uhuru msimu huu baada ya kwanza kutoa kwenye mchezo dhidi ya Azam FC lililofungwa na Mrisho Ngassa dk ya 13 na leo mbele ya Prisons.
Kiukwel kwa wazawa Kafka soka mtu ambaye mpira ni talent Ajibu ndo talented yaan sio mpira wa nguvu n automatic flexible talented player hata Manala anajua hilo
ReplyDelete