May 22, 2019


KITENDO cha mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kufunga mabao 23 kwenye Ligi Kuu Bara kimemfanya mshambuliaji huyo raia wa Rwanda kuingia kwenye rekodi moja na mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Aubameyang na Mohamed Salah wa Liverpool ambao walimaliza Ligi Kuu England wakiwa na idadi hiyo ya mabao.

Kagere aliyetua Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya kwa sasa ndiye kinara wa ufungaji mabao katika ligi kuu akifuatiwa na Salim Aiyee pamoja na Heritier Makambo.

Kagere licha ya kufunga mabao hayo ana nafasi ya kuongeza kutokana na kubakiwa na michezo mitatu ikiwemo mchezo wa jana dhidi ya Singida United.

Salah, Aubameyang pamoja na Sadio Mane wao waliweka rekodi ya kuwa vinara wa ufungaji kwenye Ligi ya England baada ya wote kwa pamoja kufunga mabao 22, ligi hiyo ilimalizika wiki chache zilizopita.

Akizungumzia juu ya hilo, Kagere anasema: “Kiu yangu siyo kufikia hapa, ninataka kuendelea kufunga zaidi ili niisaidie timu yangu lakini mimi mwenyewe kujiwekea rekodi ya kufunga katika klabu yangu. Nitaendelea kupambana zaidi na zaidi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic