May 22, 2019


NAHODHA wa Singida United, Kennedy Juma amesema kuwa bado timu yao ina nafasi ya kubaki kwenye ligi msimu ujao kwani wana mchezo mkononi watapambana kupata pointi moja.

Juma amesema kuwa walijipanga kupata matokeo mbele ya Simba ila walishindwa kutokana na kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata.

"Tumepoteza kwa kuwa tulishindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata, ila bado tuna nafasi ya kubaki kwenye ligi kwa kuwa mchezo mmoja mkononi tunao na tunahitaji pointi moja.

"Mchezo wetu unaofuata tutakuwa Tanga hivyo tutapambana kupata pointi moja ili tubaki kwenye ligi msimu ujao," amesema Juma.

Singida United imecheza michezo 37 imejikusanyia jumla ya pointi 45 ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo, mchezo wake wa mwisho itacheza na Coastal Union Tanga.

1 COMMENTS:

  1. Naona bado baadhi ya watanzania hawajaridhika na uhalali wa ubingwa aliouchukua Simba...sijui shida iko wapi? maana mimi bado sijaiona!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic