May 22, 2019

NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa siri kubwa iliyojificha kwenye ushindi wao na kuweza kutetea ubingwa msimu huu ni juhudi na nia ambayo waliiweka awali.

Simba jana walitwaa ubingwa mbele ya Singida United mchezo uliochezwa uwanja wa Namfua kwa ushindi wa mabao 2-0.

"Tunamshukuru Mungu kwa kutwaa ubingwa tena msimu huu haikuwa kazi rahisi kwani ushindani ulikuwa mkubwa ila juhudi zilitubeba.

"Mashabiki wamekuwa nasi bega kwa bega nasi tulipambana uwanjani hivyo ni jambo la furaha kwetu kuona kwamba tumetimiza malengo yetu," amesema Bocco.

Simba imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 20 huku wapinzani wao Yanga wakiwa wametwaa mara 27.

1 COMMENTS:

  1. Naona bado baadhi ya watanzania hawajaridhika na uhalali wa ubingwa aliouchukua Simba...sijui shida iko wapi? maana mimi bado sijaiona!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic